Nataka Mkataba wa miezi 12: John Terry

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mchezaji wa Klabu ya Chelsea John Terry

Nahodha wa Chelsea John Terry anataka kuendelea kuitumikia klabu yake kwa muda mrefu akitaka Mkataba wake mpya iongezwe kwa miezi 12.

Beki huyu mwenye umri wa miaka 34 Mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, akiwa amecheza michezo 656.

"Timu inafahamu nafasi yangu ninataka kusalia, na naamini kiwango changu kinaonesha wanaweza kunibakisha".Alisema Terry.

Terry alianza kuitumikia timu yake kwa kucheza mchezo wa kwanza mwaka 1998 mwezi Oktoba.