Calderon:Mourinho hakuweza presha Madrid

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa kocha wa Raal Madrid Jose Mourinho

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho hakuweza kuhimili presha kama mkufunzi wa Real Madrid ,aliyekuwa rais wa kilabu hiyo Ramon Calderon amesema.

Mkufunzi huyo wa Chelsea aliifunza kilabu hiyo kutoka mwaka 2010 hadi mwaka 2013, na hivyobasi kushinda taji la La Liga mwaka 2012 na taji la Copa Del Rey mwaka 2011 kabla ya kuelekea Stamford Bridge.

''Kuwa Meneja wa kilabu ya Real Madrid sio mchezo ni vigumu sana'',Calderon aliiambia BBC. Angalia kilichompata Mourinho.''Ni mtu ambaye hakuweza kuhimili presha'',.

Mourinho alimaliza wa pili katika La Liga katika msimu wake wa pili kama mkufunzi wa Real Madrid,ikiwa ni alama nne nyuma ya Barcelona,lakini alishinda ligi mwaka uliofuata alipoipatia Real Madrid pointi 100.