Van Persie apata jeraha

Haki miliki ya picha PA
Image caption Van Persie apata jeraha

Kilabu ya Manchester United inasubiri kujua ubaya wa jeraha la mshambuliaji wake Robin Van Persie baada ya mchezaji huyo kuondoka katika uwanja wa Liberty akitumia magongo.

Van Persie mwenye umri wa miaka 31 pia alionekana amefungwa mbamba katika mguu wake wa kulia baada ya kupata jeraha katika mda wa lala salama wa mechi dhidi ya Swansea ambapo Swansea waliibuka kidedea jumamosi.

Msimu huu Robin Van Persie ameifungia Manchester United mabao 10,lakini hakuweza kutolewa kwa kuwa United tayari ilikuwa imefanya mabadiliko matatu.