Hali ya Fernando Alonso yaimarika

Image caption Dereva wa Magari yaendayo kasi, Fernando Alonso

Hali ya Dereva wa Magari yaendayo kasi ya Fomula 1 Fernando Alonso imeimarika lakini ataendelea kubaki hospitali kwa uangalizi zaidi.

Alonso alipata ajali hiyo wakati akifanya majaribio ya magari ya timu ya Mclaren kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano ya magari.

Uongozi wa timu hiyo umesema hakuna ushahidi unaonyesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na tatizo lolote la kiufundi.

Bado hakuna maamuzi yaliyotolewa toka kwa uongozi kama dereva huyo atakuwa tayari kushiriki hatua ya tatu ya majaribio ya magari yatakayofanyika baadae wiki hii.