Kombe la dunia ni Novemba na December 2022

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Qatar na Urusi kuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 ilijulikana miaka nane iliyopita.

Michuano ya Kombe la dunia inalotarajiwa kuchezwa mnamo mwaka 2022 huko Qatar limepangwa kutimua vumbi kati ya miezi ya November na December, kikosi kazi cha Fifa kimetoa tamko .

Wakuu wa mpira wa miguu wamekutana mjini Doha kujadili juu ya masuala kadhaa ya kuchagua juu ya hali ya majira ya kiangazi endapo yataathiri afya ya wanamichezo na mashabiki wao.

Majira ya kiangazi nchini Qatar hakizidi nyuzi joto 40C na mwezi wa November na mwezi December hushuka na kufikia nyuzi joto 25.

Kikosi kazi hicho kinaongozwa na chief Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa na amesema kwamba michuano hiyo ya kombe la dunia ya mwaka 2022 inapaswa kupigwa kwa siku chache tu .

Pamoja na mipango na kauli mbalimbali tayari kuna utabiri unaoonesha kuwa michuano hiyo inaweza kuanz arasmi mnamo tarehe 26 November na kwisha tarehe 23 December.

Hata hivyo, Fifa imesema haina mpango wa kupunguza muda wa michuano hiyo kutoka timu 32 ama michezo 64 .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Qatar na Urusi walijulikana miaka minne iliyopita kuwa wenyeji wa michuano hiyo

Kwanini November-December?

Fifa imesema kwamba imeshafanya uchaguzi wa namna mbali mbali katika masuala mengi na kujadili pia lakini imeona kwamba miezi hiyo November-December ni bora zaidi na sababu za fifa ni hizi katika kutetea hoja yake .

Miezi ya January-February micguano hiyo itakwaana na michuano ya majira ya baridi ya OlympicsMwezi wan ne ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao unatarajiwa mfungo kuanza tarehe 2 April mwaka 2022Hali ya joto inatarajiwa kudumu kutoka mwezi May hadi September nchini Qatar

Katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke kumekuwa na faida na hasara ya chaguo lakini suluhisho ni miezi hiyo ya November na December.

Sheikh Salman anasema wameridhishwa, nah ii ni baada ya uzingatifu makini wa mawazo tofauti tofauti na majadiliano ya kina na wadau wa soka ,tumetambua kile tunachokitaka na ndio suluhisho la michuano ya kimataifa ya mwaka 2018-2024 na kandanda kwa ujumla wake .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nyasi zitachakazwa

Juu ya fainali kuwa 23 December?

Makamu raisi wa Fifa Jim Boyce kupeleka michuano hiyo kwenye majira ya baridi ilitumika akili ya kaida tu lakini juu ya mchezo wa fainali kupigwa tarehe 23 December itakuwa imekaribia sana sherehe za mwisho wa mwaka Christmas na tamasha la kitamaduni la Uingereza .