UEFA yaitoza faini Celtic

Haki miliki ya picha ap
Image caption Celtic

Klabu ya Celtic imetozwa faini ya paundi 7,300 na Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA.kufuatia vurugu za mashabiki wake katika mchezo wa makundi ya Europa ligi dhidi ya Dinamo Zagreb.

Hiyo inakuwa mara ya tano katika kipindi cha miaka mitatu Celtic kutozwa faini na UEFA kutokana na vurugu za mashabiki wao.

Mashabiki hao walikwaana na polisi baada ya kurusha mafataki Desemba mwaka jana.

Adhabu hiyo ya faini iliyotolewa na kamati ya maadili na nidhamu ya UEFA imekuja wakati Celtic na mashabiki wake wakisafiri kuelekea nchini Italia

kwa ajili ya mchezo wao wa mkondo wa pili wa michuano ya Uefa Europa ligi dhidi ya Inter Milan.