Alonso atashiriki Fomula1: Ron Dennis

Image caption Fernando Alonso

Boss wa timu ya magari yaendayo kasi ya Mclaren Ron Dennis amesema dereva Fernando Alonso anatarajiwa kushiriki msimu mpya wa mbio za magari za Grand Prix zitakazo fanyika Australia

Kwa sasa Alonso mwenye miaka 33 yuko nchi kwao Hispania kwa mapumziko baada ya kupata ajali.

Dennis amesema uamuzi wa mwisho kama Alonso ataweza shiriki michuano hiyo itaamuliwa na na madaktari japo anaendelea vizuri kabisa.

Alonso hatoweza kushiriki majaribio ya Magari yanayofanyika huko Barcelona na kumpelekea dereva Dane Kevin Magnussen kuwa dereva mwenza wa Jenson Button katika timu hiyo Mclaren.