Wacheza tenisi walemavu kuchuana Kenya

Image caption Mcheza Tennis wa Tanzania

Wachezaji wawili wa Tanzania wa mchezo wa tenisi kwa wenye ulemavu (Wheelchair tennis) wanategemewa kuiwakilisha nchi katika michuano ya Africa ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia kwa vilabu la BNP (BNP Paribas World Team Cup African Qualification tournament) yanayofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Kenya, ikiwa nchi mwenyeji itazikaribisha nchi za Afrika ya Kusini, Tanzania, Ghana, Morocco na Mauritius katika michuano iliyoanza leo Nairobi mpaka Jumapili.

Washindi watafuzu kucheza michuano ya timu ya dunia (BNP Paribas World Team Cup) itakayofanyika klabu ya Alibey Manavgat, nchini Uturuki kuanzia May 25 mpaka 31.

Wachezaji kutoka Tanzania ni Novatus Temba na Emmanuel Masapinib wakiwa chini ya kocha Riziki Salum, kwa mujibu wa viongozi wa Chama cha Tenisi Tanzania (TTA).