Kombe la Shirikisho:Yanga dimbani leo

Image caption Kikosi cha Yanga ya Tanzania

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Yanga Leo hii watajitupa uwanjani kuwakabili BDF XI huko Gaborone, Botswana.

Huu ni mchezo wa marudiano ambapo mchezo wa awali Yanga walishinda magoli 2-0 mchezo ulifanyika Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Jumamosi Timu nyingine mbili za Tanzania, Azam FC na KMKM, zitakuwa Viwanjani kwenye Mechi za raundi ya pili ya Klabu bingwa barani Afrika CAF

Wakati Polisi ya Zanzibar itacheza Mechi yake ya Pili ya raundi ya kwanza ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho hapo Jumapili.

Yanga na Azam FC, ambao wako Ugenini wanahitaji Sare ya aina yoyote au ushindi kuweza kusonga mbele kwa hatua inayofuata.