Arsenal kumenyana na Everton

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachezaji wa Arsenal wakikabiliaana na wenzao wa Everton wakati wa mechi kati ya timu hizo mbili

Kurudi uwanjani kwa kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere' kutacheleweshwa kwa siku chache baada ya mchezaji huyo kufanyiwa upasuaji mdogo.

Mwenzake Aaron Ramsey na Mathiew Flamini hawajulikani iwapo watacheza kufuatia majeraha ya mguu.

Upande wa Everton Romelu Lukaku anatarajiwa kuwa sawa licha ya kutoka katikati ya mechi na jeraha la mguu wiki iliopita.

John Stones na Aaron Lennon wanarudi baada ya kuhudumia marufuku lakini Steve Pienaar bado yuko nje na jeraha la goti.