Liverpool kutoana jasho na Mancity

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kun Aguero

Mchezaji wa Liverpool Phillpe Coutino anarejea uwanjani siku ya jumapili baada ya kupumzishwa katika mechi dhidi ya Besikitas lakini jeraha la mguu la Jordan Henderson litatathminiwa upya.

Beki wa upande wa kulia Glen Johnson anatarajiwa kuwa amepona baada ya kuugua huku Lazar Markovic akirudi baada ya kuhudumia marufuku.

Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure anarejea baada ya kukosa mechi ya katikati ya wiki ya kombe la vilabu bingwa Ulaya kupitia maraufuku.

Mshambuliaji Wilfried Bonny huenda akaanzishwa baada ya kuanza kama mchezaji wa ziada wikendi iliopita.