Westbrom yachapwa na Aston Villa 2-1

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chelsea mpaka sasa bado inaendelea kuongoza kwenye msimamo wa Ligi kuu ya England

Ligi kuu England, iliendelea usiku wa kuamkia leo kwa viwanja vitatu kuwaka moto. Aston Villa walikuwa wenyeji wa West Brom, hadi mwisho wa mchezo wao, wenyeji wakaibuka na ushindi wa mabao 2-1. Ushindi huo umeiondoa Aston Villa katika kundi la timu tatu za mwisho zitakazoteremka daraja. Hull City wameshindwa kutamba nyumbani kwao walipomenyana na Sunderland na kulazimishwa sare ya bao 1-1, huku Southampton ikijinyakulia pointi 3 muhimu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace. Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa Manchester City ikiwakaribisha Leicester City, wakati Manchester United watakuwa ugenini kuvaana na Newcastle. Arsenal watakuwa wageni wa QPR, huku Liverpool ikipepetana na Burnley. Katika viwanja vingine West Ham watakuwa wenyeji wa Chelsea, Totthenham wakicheza na Swansea, na Everton watasafiri kucheza dhidi ya Stoke City.