Cisse na Evans watemeana mate uwanjani

Image caption Cisse

Mlinzi wa kilabu ya Manchester United Johnny Evans na mshambuliaji wa Newcastle Papiss Cisse ni sharti wapigwe marufuku na shirikisho la soka nchini Uingereza FA baada ya kuonekana wakitemeana mate kulingana na wachanganuzi wa BBC.

Wawili hao walionekana wakitemeana mate wakati wa mechi ambapo Manchester United waliinyuka Newcastle bao 1-0.

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Newcastle Dietmer Hamann ameiambia BBC katika kipindi cha mechi ya siku kwamba wachezaji wote wawili wanafaa kupewa marufuku ya wiki kadhaa.''Hii haikubaliki ni karaha''.

Image caption Cisse

Phill Nevile alisema kuwa kutemeana mate ni kitu kibaya ambacho mchezaji anaweza kufanya uwanjani.

Beki huyo wa zamani wa kilabu ya Manchester United aliongezea:''haikubaliki kabisa.wachezaji wote wawili wataaibika watakapoona kilichokuwa kikiendelea''.

Cisse alijifuta uso baada ya kudai kutemewa mate na Evans.

Image caption cisse

Marejeleo ya kanda ya video yanaonyesha Evans akimtemea mate Cisse ambaye alikuwa uwanjani baada ya mshambuliaji huyo kumchezea visivyo raia huyo wa Ireland kazkazini.

Na baadaye raia huyo wa Senegal alionekana kumkaribia Evans na kumtemea mate.