Poyet aadhibiwa kwa kuzua purukushani

Image caption Poyet aadhibiwa na Shirikisho la FA

Kocha wa Sunderland Gus Poyet ameshtakiwa kwa kuzusha tafrani uwanjani timu yake ilipokuwa ikikabiliana na Hull City siku ya jumanne..

Shtaka hilo linafuatia mshikemshike iliyotokea uwanjani KC stadium baada ya mchezaji kiungo cha kati wa Sunderland Jack Rodwell alipolishwa kadi ya njano kwa kucheza visivyo na refarii Mike Dean.

Poyet alitahamaki na akapiga teke kichupa kilichokuwa na maji huku akimfokea kocha mwenza Bruce.

Refarii alilazimika kuingilia kati kuwazua makocha hao wawili wasilishane makonde.

Refarii Dean alimpiga marufuku uwanjani wakati huo Sunderland ikiwa nyuma bao moja kwa nunge.

Mechi hiyo hatimaye iliishia sare ya moja kwa moja.

Makocha hao wawili wamesema kuwa ilikuwa tu ni joto la wakati huohuo.

Kocha poyet anahadi siku ya jumatatu kujibu mashtaka yake ama kutoa sababu kwanini hatua kali zisichukuliwe dhidi yake.