Evans na Cisse kuadhibiwa kwa kutemeana Kohozi

Haki miliki ya picha Press Association
Image caption Cisse akimkabili Evans

Mlinzi wa Manchester United Jonny Evans na Mshambulizi wa Newcastle United Papiss Cisse huwenda wakaadhibiwa vikali baada ya kutemeana makohozi katika mechi ngumu baina yao jana usiku.

Kulingana na wandani wa maswala ya nidhamu katika ligi hiyo ya Uingereza,wawili hao huwenda wakapigwa marufuku ya mechi sita kila mmoja.

Refarii Anthony Taylor aliwaonya wawili hao lakini hakuchukua adhabu yeyote dhidi yao.

Sasas shirikisho la Kandanda la Uingereza linasubiri ripoti ya refarii huyo ilikubaini hatua ipi itawafaa vibonde hao wawili.

Msimu uliopita George Boyd alipigwa marufuku ya mechi 3 kwa kumtemea kohozi kipa ya Manchester City Joe Hart.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Refarii Anthony Taylo akiamua malumbano baina ya Evans na Cisse

Msimu huu hata hivyo sheria mpya zinasema kuwa adhabu iwe maradufu ya hiyo ili iwe ni funzo dhidi ya yeyote atakayekuwa mtundu uwanjani.

Cisse ambaye mwezi Desemba alipigwa marufuku kwa kumshambulia kiungo wa Everton Seamus Coleman.

Kwa mujibu wa wachezaji wakongwe Evans na Cisse wanastahili adhabu kali.

Meneja wa Newcastle John Carver na Louis van Gaalwa Manchester United hawakusema lolote kuhusiana na tukio hilo.