Manchester United kumuuza Di Maria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Di Maria

Di Maria hajaonyesha umahiri wake tangu aliposajiliwa katika kilabu ya Manchester united kutoka Real Madrid na inaaminika kwamba yeye na mkewe hawajazoea maisha ya Manchester baada ya jaribio la wizi katika nyumba yao.

Wiki iliopita raia huyo wa Argentina ,mkewe Jorgelina Cardoso na mwanawe wa mwaka mmoja wamehamia katika nyumba ya aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Phil Nevile iliopo ghorofa ya 45.

Wamekodisha nyumba hiyo kwa kuwa Di Maria ana mpango m'badala wa maisha yake swala ambalo kilabu ya Manchester United inalifahamu.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Gareth Bale

Hatua hiyo inadaiwa kushinikiza harakati za kilabu hiyo kutaka kumsajili mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale.

Ijapokuwa Bale amekuwa akisema kuwa hataki kuondoka katika kilabu ya Real Madrid ili kurudi katika ligi ya Uingereza,United inahisi kwamba inaweza kum'bembeleza ili kubadilisha msimamo wake iwapo watakubaliana na mabingwa hao wa Ulaya.