Mechi yavunja rekodi kuchezwa muda mrefu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mcheza tenis raia wa Argentina Leonard Mayer

Mechi ya Mchezo wa tenis kati ya raia wa Argentina Leonardo Mayer na Joao Souza wa Brazili imevunja rekodi ya mchezo huo hapo jana kwa kuwa mechi pekee ya mchezo wa tenis kuchezwa kwa muda mrefu kuliko wowote uliowahi kuchezwa katika michuano ya Davis Cup.

Katika mechi hiyo wachezaji hao walivunja rekodi iliyowahi kuwekwa mwaka 1982 katika michuano hiyo baada kutumia saa sita na dakika arobaini na mbili ambayo ni zaidi ya dakika 20 ya ile iliyovunjwa mwaka 1982.

Katika mechi hiyo Mayer wa Argentina alimfunga Joao Souza wa Brazil kwa jumla ya seti tano.