Arsenal kuivaa Bradford City au Reading

Haki miliki ya picha PA
Image caption Arsenal kupambana na Bradford City au Reading

Mabingwa watetezi wa michuano ya Kombe la FA, Arsenal wanatarajiwa kupambana na Bradford City au Reading katika hatua ya nusu fainali baada ya kuwatandika Manchester United hapo jana.

Katika mchezo mwingine wa nusu fainali ya michuano hiyo Aston Villa wao watakwaana na mshindi kati ya Liverpool au Blackburn Rovers.

Reading na Bradford zinatarajiwa kucheza mchezo wao wa marudiano wa robo fainali Machi 16 huku mchezo baina ya Blackburn na Liverpool ukiwa bado haujathibitishwa siku utakayochezwa.

Mechi za nusu fainali zote zinatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Wembley April 18 na 19 mwaka huu.