Real Madrid, Porto robo fainali UEFA

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mshambuliaji wa Real Madrid aliyevunja rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye michuano ya Klabu bingwa Ulaya

Pamoja na Real Madrid kufungwa hapo jana na Schalke 04 ya Ujerumani kwa magoli 4 - 3 katika mechi ya klabu barani ulaya timu hiyo imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano hiyo.

Real Madrid imenufanika na matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza ambapo iliwalaza Schalke 04 kwa jumla ya magoli 2- 0 na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla ya magoli 5 - 4.

Hapo jana Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo alivunja rekodi kuwa mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi katika michuano hiyo.

Ronaldo alifunga magoli 2 kati ya matatu ya Real Madrid na kufikisha jumla ya magoli sabini nane na hivyo kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ya Real Madrid, Raul.

Mchezaji anayemfuatia kwa karibu kwa kufunga mengi katika michuano hiyo kwa sasa ni Lionel Messi ambaye hadi sasa ana magoli sabini na tano kwenye michuano hiyo.

Na katika mechi nyingine iliyopigwa hapo jana FC Porto ya Ureno nayo imeingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuibamiza timu ya FC Basel ya uswis kwa magoli manne kwa mtungi.

Katika mechi ya awali timu hizo zilitoka sare ya goli moja kwa moja na hivyo FC Porto kuingia robo fainali kwa jumla ya magoli

Na leo kutakuwa na mechi nyingine za michuano hiyo ambapo Chelsea wanakaribisha Paris St Germain ya Ufaransa katika uwanja wa Stamford Bridge huku huku Bayern Munich wakipepetana na Shakhtar Donetsk ya Ukraine.