Chelsea Paris St Germany dimbani leo UEFA

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Psg na chelsea

Timu ya soka ya Chelsea itashuka katika dimba lake la Stamford Bridge kuwakaribisha Paris St Germany katika mchezo wa klabu bigwa ulaya.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchi Ufaransa timu hizi zilikwenda sare ya kufungana bao 1-1.

Kiungo Nemanja Matic anatarajiw kurejea katika mchezo huu huku John Mikel Obi hatokuwepo katika kikosi hicho sababu ya maumivu ya goti.

Mchezo mwingine utakua ni kati ya Bayern Munich dhidi ya Shakhtar Donetsk mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Allianz Arena.

Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilienda sare ya bila kufunga .