Arsenal yaicharaza West Ham 3-0

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Arsenal yaifunga West ham mabao 3-0

Arsenal ilipata ushindi mzuri dhidi ya West Ham huku ikijiandaa kwa mchuano wa kata na shoka kati yake na kilabu ya Monaco siku ya jumanne.

Kilabu hiyo ya Wenger iliishinda West Ham kwa mabao 3-0 na hivyobasi kuimarisha ndoto yake katika nafasi nne bora katika jedwali la ligi ya Uingereza.

The Gunner ilitawala mechi hiyo huku Olivier Giroud akifunga bao la kwanza kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Kevin Nolan na Matt Jarvis walikaribia kufunga kwa niaba ya wana nyundo hao lakini mabao ya dakika za mwisho ya Aaron Ramsey na Mathiew Flamini yaliiiweka Arsenal pointi nne mbele ya mabingwa wa zamani Manchester United walio katika nafasi ya nne.

Arsenal sasa inajianda kubadilisha matokeo ya 3-1 dhidi ya Monaco nchini Ufaransa siku ya jummane katika mechi ya vilabu bingwa barani Ulaya.