Raheem Sterling:Liverpool yapata pigo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Raheem Sterling amekataa kuanzisha mazungumzo mapya ya mkataba wake

Kilabu ya Liverpool imepata pigo baada ya mshambuliaji nyota Raheem Sterling kukataa kuanzisha mazungumzo juu ya mkataba mpya ,hadi mkataba wake utakapokamilika.

Sterling ambaye amekuwa mchezaji nyota wa kilabu hiyo msimu huu amevivutia vilabu vya Real Madrid na Chelsea.

Vilabu vyote viwili vinadaiwa kujiandaa kumnunua mchezaji huyo msimu huu ,na huku Liverpool ikijaribu kupata sahihi yake kwa lengo la kuongeza mkataba wake,Sterling amesitisha mazungumzo kuhusu mkataba huo.

Kulingana na gazeti la the Mirror,mchezaji huyo amesema kuwa hataanzisha mazungumzo hadi mwisho wa msimu huu,swala ambalo linaonekana kuwa pigo kubwa upande wa Liverpool.

Kwa sasa Sterling anapokea mshahara wa pauni 35,000 kwa wiki na amedai kukataa mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki mwezi uliopita.