Monaco hawakustahili kusonga mbele

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Anafahamika kama Arsene Wenger,meneja wa klabu ya Arsenal.

Meneja wa klabu ya soka ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger anaamini timu ya Monaco haikustahili kusonga mbele kwenye hatua ya nane bora ya ligi ya mabigwa ulaya.

Licha ya Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Monaco walishindwa kufuzu kwa nane bora baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kuchapwa 3-1.

Kocha Wenger amesema haamini kama timu hiyo ilitakiwa kusonga mbele “ukiangalia idadi ya mashuti yaliyolenga goli utashangaa, kupoteza mchezo kunauma ila hatujapoteza."

Hii imekua ni mara ya tano mfululizo kwa washika bunduki hao wa London kushindwa kufuzu hatua ya nane bora.