sheria ya magoli ya ugenini irekebishwe

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsene Wenger

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema sheria ya mabao ya ugenini inapaswa kutumika baada ya muda wa nyongeza kuliko katika muda wa kawaida kama ilivyo sasa.

Arsenal walienguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa sheria ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Monaco ya Ufaransa.

Timu hiyo ilipoteza mchezo wao wa kwanza kwa kufungwa mabao 3-1 Februari 25 mwaka huu kabla ya kujirudi na kuifunga Monaco mabao 2-0 katika mchezo wao wa maridiano uliofanyika katika Uwanja wa Louis 11 Juzi.

Wenger amesema sheria hiyo ilitungwa katika miaka ya sitini na uzito wa bao la ugenini hivi sasa ni mkubwa.

Bao la ugenini huwa linahesabika baada ya muda wa nyongeza katika mechi za mkondo wa pili kwenye michuano ya Kombe la Ligi hatua ya nusu fainali lakini kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League sheria hiyo hutumika baada ya muda wa kawaida wa dakika 90 kumalizika.

Wenger amesema timu mbili za Uingereza zimeondolewa katika michuano hiyo kwa sheria ya bao la ugenini jambo ambalo wahusika wanapaswa kujiuliza nap engine kuangalia upya sheria hiyo.

Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wakati sheria hiyo ikitungwa katika miaka ya sitini ilikuwa na dhumuni ya kuzifanya timu kushambuliana lakini soka hivi sasa limebadilika.