Liverpool kumenyana na Manchester United

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption LIverpool kumenyana na Manchester United uwanjani anfield

Kiungo wa kati wa kilabu ya Liverpool Lucas Leiva amerudi katika mazoezi baada ya kukaa wiki tano nje na jeraha la mguu lakini hayuko tayari kucheza dhidi ya Manchester United.

Mshambuliaji Mario Balotelli amepona ugonjwa uliomfanya kukosa mechi ya ushindi dhidi ya Swansea siku ya jumatatu.

Kiungo wa kati wa Manchester United ambaye pia ni mchezaji nyota Angel Di Maria atacheza baada ya kuhudmia marufuku ya mechi moja lakini Jonny Evans bado anahudumia marufuku.

Mlinzi Luke Shaw na Marcos Rojo huenda wakarudi baada ya kuuguza jereha lakini wote hawajaimarika kuanza katika kikosi dhidi ya Liverpool.