England kuandaa kombe la dunia 2026 ?

Haki miliki ya picha
Image caption Sepp Blatter Rais wa FIFA

England sasa inafikiria kuingia katika kinyanganyiro cha kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2026 baada ya kujaribu bahati hiyo ilii iandae fainali hizo mwaka 2018 lakini ilijikuta ikitupwa nje baada ya kupata kura mbili na kuiacha Urusi ikibeba jukumu hilo.

Hata hivyo mwenyekiti wa shirikisho la kandanda England Greg Dyke, amesema jaribio lao litategemea kama rais wa FiFa Sepp Blatter ataendelea kusalia madarakani.

Greg amesema kuteuliwa kwa mwingereza David Gill katika kamati ya kuu ya uongozi ya Fifa inaweza kuongeza ushawishi.

Hata hivyo Greg amesema England itachukua hatua hiyo iwapo tu sera zitakuwa wazi lakini hataitaomba kuwa mwenyeji wa fainali wakati Blatter akiwa bado yupo madarakani.