Uganda na Tanzania kuchuana :kriket

Image caption Timu ya Kriketi ya Tanzania

Tanzania imepangwa kucheza na Uganda katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya Afrika Ligi Daraja la 1 itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini katika mji wa Benoni mwishoni mwa wiki hii.

Chama cha Kriketi nchini Tanzania kimeteua timu ya taifa kwa ajili ya michuano hiyo na tayari timu hiyo imeondoka Tanzania kuelekea Afrika ya Kusini.

Nahodha wa Tanzania, Hamisi Abdallah amesema Uganda sio timu ngeni na wanaichukulia mechi yao kwa umuhimu mkubwa.Nchi nyingine zinazotegemewa kushiriki michuano hiyo ni Kenya, Namibia, Botswana na Ghana.

Abdallah anaendelea kuwa nahodha wa timu hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja (miaka 10) akiwa na uzoefu wa kutosha wa michuano ya kimataifa, huku akiwa na rekodi ya kucheza kriketi nchini Uingereza katika klabu ya Watford Town.

Wachezaji wengine waliochaguliwa katika timu hiyo ni Abhik Patwa, akiwa na rekodi ya kufunga nusu century ( runs 50) katika michuano iliyopita ambapo Nigeria na Ghana waliibuka vinara.

Wachezaji wengine ni Yakesh Patel, Ally Mpeka, Arshan Jassani, Riziki Kiseto, Zamoyoni Jabeneke,Harsheed Chohan, Issa Kikasi,Kassim Nassoro, Arun Dagar, Khalil Rehemtullah,Martin Mwarabu na Rahil Amarshi,