John Terry aongezewa mkataba Chelsea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nahodha wa Chelsea John Terry aongezewa mkataba

Nahodha wa kilabu ya Chelsea John Terry ameongeza mkataba wake katika kilabu hiyo hadi mwisho wa msimu wa mwaka 2015-16.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34,ambaye mkataba wake wa awali unakamilika mwisho wa msimu huu ameichezea Chelsea mara 550.

Chelsea wanaongoza kwa pointi sita katika jedwali la ligi ya Uingereza wakiwa na mechi moja zaidi ambayo hawajacheza dhidi ya wapinzani wao na mkufunzi Jose Mourinho anasema kuwa kandarasi hiyo ya mwaka mmoja si ya kumpatia asante John Terry bali ni kwa sababu anaendelea kucheza vizuri.

Ni mlinzi wa kiwango cha juu.

Mourinho hivi majuzi alisema kuwa ana hakika kwamba Terry atapewa mkataba mpya,ikiwa ni miongoni mwa sera za kilabu hiyo kuwaongezea kandarasi awchezaji ambao wamepitisha umri wa miaka 30.