Sebastian Vettel amuangusha Hamilton

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sebastian Vettel,dereva wa timu ya Ferrari
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes

Dereva wa mbio za magari wa timu ya Ferrari Sebastian Vettel amembwaga Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes na kufanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza akiwa na timu hiyo katika mashindano ya Malaysian Grand Prix. Vettel ameshinda katika shindano ambalo lilikuwa kali na la kusisimua baada ya Hamilton kuharibikiwa na tairi kutokana na joto lililotokana na hali ya hewa ya kitropic na kufanya dereva huyo kushika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikienda kwa Nico Rosberg. Ushindi wa mjerumani huyo umemfanya kuwa ndiye dereva mwenye mafanikio makubwa katika eneo la Sepang akiwa na mataji manne huku akiwa ni wa 34 wa tofauti katika timu ya Ferrari.