Mashindano kusaka nafasi Ulaya yaendelea

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wachezaji wa timu ya Wales

Patashika ya kutafuta tiketi ya kufuzu mashindano ya soka ya mataifa ya Ulaya yanayotaraji kufanyika mwakani iliendelea jana kwa michezo kadhaa kupigwa. Ureno walikuwa wenyeji dhidi ya Serbia hadi kipyenga cha mwisho Serbia imeangukia pua kwa kufungwa mabao 2-1. Wakati hayo yakijiri, Hungary imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana walipocheza dhidi ya Ugiriki, mabingwa wa dunia Ujerumani imeiadhibu Georgia kwa mabao 2-0, huku Ireland ya kaskazini ikiirarua Finland kwa jumla ya mabao 2-1. Scotland ikaisambaratisha Gibraltar kwa ushindi wa mabao 6-1 wakati Jamhuri ya Ireland ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya Poland.