Steven Fletcher atoa mwiko wa Hat trick

Image caption Steven Fletcher

Mchezaji Steven Fletcher ameifungia timu yake ya taifa ya Scotland hat-trick ya kwanza baada ya miaka 46 pale walipocheza dhidi ya Gibraltar.

Mchezaji wa mwisho kufunga hat-trick katika timu hiyo alikuwa ni Colin Stein ambapo alifunga magoli 4 mnamo mwaka 1969 pale walipocheza dhidi ya Cyprus. Katika mchezo huo wa jana ambao uliisha kwa ushindi wa jumla ya mabao 6-1 umeikumbusha Scotland ushindi mnono ulioupata mwaka 2006, iliposhinda mabao 6-0 dhidi ya Faroe Islands.

Fletcher mwenye umri wa miaka 28 ni mchezaji wa kimmataifa ambaye anakipiga ligi kuu ya England ndani ya klabu ya Sunderland.