Sibtain Kassamali mteuzi mkuu Kenya

Image caption Kocha Sibtain Kassamali

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya kriketi ya Tanzania, Sibtain Kassamali ameteuliwa na bodi ya kriketi ya Kenya kuwa mteuzi mkuu wa timu za Kenya katika ngazi zote (timu za vijana na wakubwa ) kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

Kassamali, aliyeifundisha Tanzania kati ya mwaka 1992 na 2001 akifanikiwa kuifikisha katika ngazi za kufuzu kucheza kombe la Dunia kwa ngazi ya Afrika, kwa sasa anafanya kazi za kriketi katika Pwani ya Mombasa Kenya, ambapo ndio asili yake.

Kassamali, ambaye ni nahodha wa zamani wa Kenya akiwa na rekodi ya kucheza mechi nyingi na kufunga zaidi ya runs (mikimbio) 1,000, amefurahia uteuzi huo na kusema ni changamoto kwake.

Uteuzi wake unakuja wakati ambapo Kenya ipo katika mkakati wa kurudisha hadhi yake katika michuano ya kombe la Dunia.