Wachezaji wa Fenerbahce washambuliwa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption shambulio la basi la kilabu ya fenerbahce

Basi la kilabu ya Fenerbahce lilifyatuliwa risasi na wapiganaji baada ya kilabu hiyo ya Uturuki kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi kilabu ya Rizespor.

Dereva wa basi hilo alipelekwa hospitalini lakini hakuna mchezaji aliyejeruhiwa wakati wa shambulio hilo ambalo lilitokea wakati walipokuwa wakielekea katika uwanja wa ndege wa Trabzon.

Waziri mkuu wa taifa hilo Ahmet Davutoglu amesema kuwa uchunguzi unaendelea.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Basi la kilabu ya fenerbahce nchini Uturuki

Shrikisho la soka nchini Uturuki lilishtumu shambulio hilo huku katibu mkuu wa kilabu hiyo Mahmut Uslu akisema kuwa kitendo hicho ni cha makosa.

''Tulikuja hapa kucheza soka'', alisema Uslu ambaye alikuwa katika basi hilo wakati wa shambulio hilo.