Pellegrini:Mancity haipo katika mgogoro

Haki miliki ya picha z
Image caption Pellegrini

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesisitiza kuwa kilabu yake haiko katika mgogoro .

Raia huyo wa Chile anatapatapa kukoa kazi yake kama mkufunzi huku timu hiyo ikipambana na Manchester United siku ya jumapili katika mechi ya debi itakayochezwa uwanjani Old Trafford.

Manchester City imeshuka hadi nafasi ya nne kufuatia msururu mbaya wa matokeo baada ya kushinda mara mbili pekee kati ya mechi saba.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Pellegrini

Kocha Pellegrini amewaona wapinzani wake Arsenal na Manchester United wakipanda katika jedwali katika majuma ya hivi karibuni na sasa anajua kwamba atasalia kuwa mkufunzi wa kilabu hiyo iwapo atafanikiwa kuiweka timu hiyo katika nne bora zitakazofuzu katika mashindano ya kuwania kilabu bingwa Ulaya msimu ujao.

Image caption Wachezaji wa Mancity

Baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo tayari wameanza kuhusishwa na uhamisho katika timu nyengine huku Pellegrini pia akiwa hajui iwapo atanedelea kufunza timu hiyo msimu ujao.

Na sasa anakabiliwa na kibarua kigumu cha kukabiliana na mahasimu wao wa jadi siku ya jumapili ambao wameshinda mechi zao za mwisho sita .