Arsenal yashinda huku Tottenham ikilazwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchezaji Aaron Ramsey akisherehekea bao alilofunga

Bao la mapema lililofungwa na mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey lilitosha kuisaidia Arsenal kupunguza mwanya uliopo kati yake na viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea hadi pointi nne.

Arsenal hatahivyo wamecheza mechi mbili zaidi ya Chelsea ambao wanacheza na QPR siku ya jumapili huku madai kwamba kinyang'anyiro hicho ni kati ya Arsenal na Chelsea yakipuuziliwa mbali.

Hatahivyo vijana wa Wenger wanaipa presha Chelsea ikilinganishwa na timu yoyote ile katika ligi hiyo baada ya kupata ushindi wa nane mfululizo na kuwa timu ya kwanza nchini Uingereza kuweza kufanya hivyo msimu huu.

Matokeo mengine

Swansea 1 - 1 Everton

Southampton 2 - 0 Hull

Sunderland 1 - 4 Crystal Palace

Tottenham 0 - 1 Aston Villa

West Brom 2 - 3 Leicester

West Ham 1 - 1 Stoke