Raha ya mechi bao,furahia ushindi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Louis Van Gaal akipeana mkono na Van Persie

Baada ya ushindi wa magoli 4-2 iliyoupata Manchester Utd mwishoni mwa wiki uliyopita dhidi ya majirani zao Manchester City katika mchezo wa ligi kuu ya England, meneja wa mashetani wekundu Louis van Gaal amesema ushindi huo ni zawadi tosha kwa mashabiki wa timu hiyo. Katika mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wa timu zote mbili, wageni Man City ndio waliokuwa wa kwanza kundika bao kupitia mchezaji wake Kun Aguero ambaye ndiye mfungaji wa magoli yote kwa upande wa City, goli la Ashley Young, Marouane Fellaini, Juan Mata na Chris Smalling yalitosha kabisa kuikusanyia Manchester Utd point tatu muhimu.

Ligi hiyo inaendelea tena leo hii kwa mchezo mmoja kupigwa pale Liverpool itakapowakaribisha Newcastle Utd. Chelsea bado inaendelea kushika usukani wa ligi hiyo wakiwa na point 73, wakifuatiwa na Arsenal yenye point 66. Manchester Utd wanashika nafasi ya tatu kwa jumla ya point 65, wakati Manchester City wakibaki nafasi ya nne wakiwa na point 61.