Kocha aomba mechi za majaribio

Image caption Kujipima uwezo ni muhimu

kocha wa timu ya taifa ya soka ya wanawake nchini Tanzania ameomba kuandaliwa mechi za kirafiki za kimataifa ili kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) .

Rogasian Kaijage ameliomba shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania kufanya mipango ili wacheze na nchi kama Zimbabwe, Afrika ya Kusini au Nigeria.

Ombi hilo ni sehemu ya ripoti ya timu hiyo iliyotolewa na kocha huyo baada ya kumaliza mchakato wa kufuzu.

Twiga imeitoa Zambia katika hatua za mchujo na sasa inajiandaa na safari ya Congo Brazzavile mwezi wa Septemba kwa michuano hiyo ya michezo ya Afrika

Twiga imefuzu kwa jumla ya mabao 6-5, kufuatia ushindi wake wa awali wa 4-2 ulioupata katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Lusaka.

Michuano hiyo ya Michezo ya Afrika itashirikisha timu katika michezo mbalimbali, ikishirikisha timu za Afrika.