Maria Sharapova aitema Fed Cup

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maria Sharapova

Mcheza tennis nambari mbili duniani Maria Sharapova hatocheza mchezo wa nusu fainali mwishoni mwa wiki hii dhidi ya mjerumani katika mashindano ya Fed Cup yanayofanyika huko Sochi nchini Urusi. Sharapova mwenye umri wa miaka 27 ameondolewa katika mashindano hayo kutokana na kusumbuliwa na jeraha la mguu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Sharapova ameonesha masikitiko yake kutokana na namna alivyokuwa na hamasa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo. “ mimi na timu yangu tulibadilisha ratiba ya mazoezi ili kuweza kuiwakilisha nchi yangu katika hatua ya nusu fainali” alisema Sharapova. " kwa bahati mbaya nimepata jeraha la mguu na haliniruhusu kuwa tayari katika mpambano huu” aliongeza mchezaji huyo.