Azam yaipa Yanga nafasi ya ubingwa

Image caption Yanga kwa raha zao

Kicheko kinaendelea kutawala katika klabu ya Yanga baada ya sare kuendelea kuitesa Azam FC katika mechi ya tatu mfululizo hivyo kuipa Yanga nafasi ya ubingwa.

Azam , katika mechi ya leo iliyochezwa mkwakwani mjini Tanga, imetoka droo ya 0-0 na wenyeji Mgambo Shooting.

Katika mechi iliyopita, mabingwa hao watetezi walitoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, ikiwa ni juma moja tu baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mbeya City.

Sare hizo zinaipa Yanga nafasi ya ubingwa kwa tofauti ya pointi 7.

Kocha was Yanga, Hans Pluijm amenukuliwa name vyombo vya habari akisema, anahitaji mechi tano tu kushinda ili kuwa mabingwa.

Yanga, ikiwa na kibarua cha mechi ya Shirikisho barani Afrika dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia hapo Jumamosi jijini Dar es Salaam, inaongoza ligi ikiwa na pointi 46 katika mechi 21 ilizocheza wakati Azam inafuatia ikiwa na pointi 39.

Logo hiyo inaelekea ukingoni kuisha hapo mwezi Mei