Bayern yaangukia pua,Barcelona kidedea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption mambo ya viwanjani kila mmoja kwa namna ya ushangiliaji wake wa goli.

Mechi za klabu bingwa barani Ulaya katika hatua ya robo fainali ziliendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa michezo miwili kupigwa. Bayern Munich walikuwa ugenini kukipiga na FC Porto ya Ureno. Katika hali isiyotarajiwa na wengi Bayern imeangukia pua kwa kucharazwa mabao 3-1.

Nako nchini Ufaransa wenyeji Paris Saint German ilishuka dimbani kuikabili miamba ya soka ya Hispania Barcelona. Katika mchezo huo wenyeji PSG wamejiweka katika hali ngumu baada ya kucharazwa mabao 3-1. Bao la Neymar jr na mawili ya Luis Suárez yalitosha kuwazamisha wenyeji wao na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Timu zote nne zitacheza michezo ya marudiano April 21 siku ya Jumanne.