Majeruhi Yanga kuikabili Etoile du Sahel

Image caption Andrey Coutinho

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazil Andrey Coutinho huenda akawa sehemu ya mchezo kati ya klabu yake na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mechi ya Shirikisho Afrika hapo Jumamosi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, Juma Sufiani, majeruhi wa Yanga, akiwemo Jerryson Tegete na Salum Telela wanaendelea vizuri na kucheza au kutocheza itakuwa ni maamuzi ya kocha.

Yanga inaendelea na mazoezi Da es Salaam kujiandaa na mechi hiyo ya kwanza.

Etoile du Sahel ya Tunisia inategemewa kuwasili Dar es Salaam Alhamisi kwa ajili ya mechi hiyo na watafanya mazoezi Ijumaa katika uwanja wa Taifa kujiweka tayari na mchezo huo.

Mechi ya marudiano itachezwa Tunis, Tunisia baada ya wiki mbili.