Nico Rosberg atamani kumbwaga Hamilton

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nico Rosberg atamani kumbwaga Louis Hamilton

Dereva wa timu ya Mercedes mjerumani Nico Rosberg amesema ni muhimu kwake yeye kwa mara ya kwanza kumaliza mashindano akiwa mbele ya dereva mwenzake wa timu hiyo Lewis Hamilton. Rosberg ameongeza kuwa, ni vema kumshinda Hamilton mwaka huu katika shindano la Bahrain Grand Prix hapo siku ya Jumapili.

Mjerumani huyo anamfuatia Hamilton kwa point 17 baada ya mashindano matatu na hakuwahi kushindwa kufudhu japo hajawahi pia kumaliza akiwa mbele ya Lewis katika mwa huu wa 2015.

‘‘Sifikirii kama naweza kumshinda Hamilton hapa, lakini pia nilifikiri hivyo katika mashindano mawili yaliopita na haikuwa hivyo” alisema Rosberg.

“ nipo hapa kujaribu kumshinda na kiukweli napenda sana uwanja huo” aliongeza mchezaji huo.

Lewis Hamilton ambaye ni bingwa wa dunia mara mbili wa mbio za magari, ameshinda mashindano manane kati ya kumi akianzia shindano la Italian Grand Prix mnamo September mwaka jana na pia amemshinda Rosberg mara nne mfululizo ikiwemo fainali za msimu uliopita huko Abu Dhabi.