Wenger:Walcott kusalia Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Walcott na mkufunzi Arsene Wenger

Meneja wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger ana imani kwamba Theo Walcot ataweka mkataba mpya na kilabu hiyo ya Ligi ya Uingereza.

Walcot mwenye umri wa miaka 26 amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake na anahusishwa na uhamisho wa kujiunga na kilabu ya Liverpool.

Alipoulizwa kuhusu kusalia kwa Walcot katika uwanja wa Emirates,Wenger alisema kuwa nina imani kuwa Walcot ana maisha mazuri mbeleni.

Mshambuliaji huyo ameanza mechi tano pekee msimu huu huku akiendelea kuuguza jeraha la mguu alilopata msimu uliopita.

Lakini mchezaji huyo wa Uingereza ambaye amefunga mabao 77 katika mechi 203 alizochezea Arsenal huenda akajumuishwa katika kikosi cha mechi ya semi fainali ya kombe la FA dhidi ya Reading.

''Amerudi kutoka katika jeraha baya sana na kila wiki anaimarika'',Wenger alisema.