Kombe la FA:Arsenal kuchuana na Reading

Image caption Mechi ya semi fainali ya FA kati ya Reading na Arsenal

Pavel Pogrebnyak atashiriki katika mechi ya semi fainali ya kombe la FA kati ya Reading na Arsenal baada ya kupona jeraha la mguu.

Naye Nathan Ake na Kwesi Appiah hawatashiriki lakini Nathaniel Chalobah na Jamie Mackie wanaweza kucheza.

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere huenda akaanzishwa kwa mara ya kwanza baada ya kupona jeraha la kifundo cha mguu.

Hatahivyo Mike Arteta na Alex Oxlaide Chamberlain bado wanauguza majeraha.

Woljciech Szczesny ataanzishwa katika goli la Arsenal.

Mlinzi wa Ufaransa Mathiew Debuchy pia huenda akaorodheshwa katika kikosi hicho,baada ya kuwa nje tangu mwezi Januari ambapo alifanyiwa upasuaji wa bega lake.