Droo:Barcelona kuchuana na Bayern Munich

Haki miliki ya picha
Image caption kilabu bingwa Ulaya

Klabu ya Barcelona Itakutana na Bayern Munich katika nusu fainali ya kwanza ya kombe hilo.

Nusu fainali ya pili itazikutanisha timu za Real madrid dhidi ya Juventus ikiwa ni mkutano wa kwanza kati ya klabu hizo mbili tangu mwaka 2003.

Nusu fainali hizo zitachezwa tarehe tano na sita ya mwezi Mei huku mechi ya marudio ikichezwa wiki moja baadaye.

katika ligi ya Yuropa,mabingwa watetezi Seville kutoka Uhispania watakabiliana na Fiorentina huku Napoli wakikabiliana na Dnipro kutoka Ukraine.