Ligi ya England timu 20 kushuka dimbani

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Timu ya Chelsea

Jumla ya timu 20 zinazoshiriki ligi ya England zinatarajiwa kushuka dimbani mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo mechi ya Chelsea na Arsenal ,inaoonekana kuwa na mvuto zaidi kwa wengi, kufuatia matokeo ya mechi hiyo kutoa picha mbili tofauti, moja kuihakikishia Chealse ubingwa iwapo itashinda mechi hiyo,na pia Arsenal ikishinda italeta mazingira ya wazi kwa timu yoyote kati ya timu hizo mbili kutwaa ubingwa.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Kocha wa Liverpool,Brendan Rodgers

Naye kocha Liverpool Brendan Rodgers ameibuka na kutamba kuwa yeye ni kocha bora na hakuna kama yeye, huku akisema anamatumaini ya kuendelea kukinoa kikosi.

Pamoja na majigambo hayo Rodgers ameweka rekodi mpya ndani ya klabu hiyo kwa kuongoza misimu mitatu bila kuchukua taji lolote, tofauti na watangulizi wake tangu mwaka 1950.