Man United yalimwa,Chelsea yatoka sare

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Louis van Gaal

Manchester United ilikosa fursa ya kupanda juu na pointi kumi dhidi ya Liverpool baada ya kulazwa mabao matatu bila na kilabu ya Everton.

United wangeongeza mwanya uliopo kati yao na Liverpool katika kinyanganyiro cha kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Lakini mabao ya James Mc Carthy na John Stone yaliiweka Everton kifua mbele kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chelsea yasherehekea matokeo ya mechi ya Arsenal dhidi yao.

Kelvin Mereiles aligonga msumari wa mwisho katika jeneza la United alipofunga bao la tatu.

Wakati huohuo Chelsea imeimarisha harakati zake za kutaka kushinda ligi ya Uingereza baada ya kutoka sare ya bila kwa bila na Arsenal katika uwanja wa Emirate na hivyobasi kuhakikisha kuwa wanasalia pointi kumi mbele ya uongozi wa ligi hiyo.