Kenya,Ethiopia zang'ara London marathon

Image caption Eliud Kipchoge mshindi wa mbio za London Marathon

Eliud Kipchoge mwanariadha kutoka Kenya ameibuka kuwa bingwa wa mbio za London Marathon mwaka huu muda mchache uliopita.

Kipchoge amemaliza maili 26 ndani ya muda wa saa mbili, dakika nne na sekunde 42.

Ameikaribia rekodi ya Mkenya mwenzake Wilson Kipsang ambaye ameshika nafasi ya pili.

Image caption Tigist Tufa mshindi wa mbio za London marathon upande wa wanawake

Kwa upande wa wanawake Tigist Tufa wa Ethiopia ameibuka kuwa kinara wa London Marathon.

Jumla ya wanariadha wasio wa kulipwa wapatao elfu 38 wameshirikia kwenye mbio hizo katika hatua ya awali.

Mbio hizo zimekusanya mamilioni ya fedha kwaajili ya msaada.