Kenya kutimua vumbi Tanzania-zig zag

Image caption Gari la mashindano

Mashindano ya mbio za magari ya Tanzania, yanayojulikana kama "Zig Zag" yanategemewa kufanyika mkoani Tanga, Kaskazini mwa Tanzania May 3 huku washiriki zaidi ya 40, wakiwemo Wakenya watatu wakishiriki.

Washiriki 20 wanategemewa kuwa wenyeji akiwemo bingwa mtetezi, Gurpal Sandhu kutoka Arusha, kwa mujibu wa waandaaji.

Washiriki kutoka Kenya waliothibitisja kushiriki ni Yusuf Pasta, ambaye anaendesha gari aina ya Subaru Impreza N10, Janmohamed Abdilatif na Farhan Khan, wote wakiendesha Subaru GCB.Wanategemewa kuwa na wasaidizi wao (navigators).

Mbio hizo zinategema kuanzia Tanga Beach Resort kuelekea Pongwe, Mkanyageni na Mjesani na kurudi zilipoanzia.