Michuano ya gofu Afrika kufanyika Zambia

Image caption Mcheza golfu katika michuano ya Afrika Mashariki

Michuano ya Afrika ya golf kwa vijana chini ya miaka 18 itafanyika mwezi May nchini Zambia na Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo zinakusudia kushiriki.

Klabu ya gofu ya Lusaka ndio itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Afrika ya vijana yatakayofanyika kuanzia May 2-8 baada ya kuteuliwa na Shirikisho la mchezo huo barani Africa (AGC).

Makamu mwenyekiti wa chama cha gofu nchini Tanzania (TGU), Joseph Tango amekaririwa akisema kuwa jitihada zinafanyika ili wachezaji wake washiriki michuano hiyo mikubwa.

Gofu itakuwa ni sehemu ya michezo itakayoshindaniwa katika michezo ya Olimpiki hapo mwakani nchini Rio de Janeiro na michezo hiyo itakuwa ni kama sehemu ya maandalizi, ambapo kwa mujibu wa Tango, Tanzania inategemewa kwenda Brazil na maandalizi yameanza kwa vijana wa vilabu mbalimbali kufanya mazoezi.

Miongoni mwa nchi zinazotegemewa kushiriki michuano hiyo ya Afrika nchini Zambia ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Afrika ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na nyingine wakiwemo wenyeji, Zambia.